Hatua za Kufuata ili Kupakua Application ya Good Doctor App

Zifahamu hatua za kufuata ili kupakua Application ya Good Doctor App ili wakati wowote utakapohitaji huduma ya afya uweze kumpata Daktari sahihi anaehusika na  changamoto yako, aliyepo katika mkoa uliopo( Karibu na wewe) na ili uweze kumuona kwa muda sahihi kwako bila kupanga foleni, kwa kufanya booking kupitia Good Doctor App.

  1. Fungua Playstore kama unatumia simu ya Android AU Apple store kama unatumia iPhone
  2. Andika Good Doctor Patient’s App kwenye eneo la search app.
  3. Chagua Good Doctor Patient’s App.
  4. Kisha, download na ku-install
  5. Then,bonyeza ‘Allow Good doctor to send notifications’
  6. Chagua lugha uipendayo kati ya Kiswahili,English au French
  7. Chagua unahitaji matibabu  Ndani ya nchi au nje ya nchi.(chagua moja kati ya hizi huduma kwa lengo la kukamilisha usajili).

NOTE:Ukishajisajili unaweza tumia huduma yoyote ya Ndani au Nje ya nchi

  • Ingiza E-mail yako ambayo ipo active
  • Ingiza password ya kuanzia ambayo ni 123 (Baadae utabadilisha na kuweka ya kwako ambayo ni siri yako)
  • Pitia vigezo na masharti (Terms and conditions) kisha bonyeza kukubali (I agree)
  • Then, bonyeza SIGN IN
  • Baada ya hapo utatumiwa OTP kwenye E-mail yako.
  • Ingia kwenye E-mail yako kisha utaikuta OTP kwenye inbox au spam
  • Copy hiyo OTP na ibandike kwenye Good Doctor App.
  • Baada ya hapo utakuwa umeingia kwenye App
  • Kisha,Bonyeza kwenye duara la juu upande wa kushoto kwenye profile ,kisha chagua account settings.
  • Hapo utaweza kuset account yako kwa kubonyeza alama ya karamu na kuweka majina yako,Jinsia,Tarehe ya kuzaliwa,number ya simu na eneo unaloishi,then bonyeza SUBMIT kuwasilisha taarifa zako.
  • Pia unaweza kubadili password yako kwa kubonyeza alama ya kufuli,weka password ya zamani(123),kisha weka password mpya (Siri yako) na kusave
  • Na pia unaweza weka profile picture yako kwa kubonyeza alama ya bahasha,chagua au piga picha na kusave
  • Hapa utakuwa umekamilisha kujisajili na kumbuka kutunza password yako na kuwa ni siri yako.

Kwa maelezo zaidi juu ya good doctor app waweza wasilina na dawati la huduma kwa wateja kwa number 0793-933-933 au 0758-583-583 au waweza kufika katika ofisi za Good Doctor App zinazopatikana jijini Dar es salaa,Posta mpya katika jengo la Haidery plaza,Ghorofa ya pili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top